TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI TCB 08-07-2020

OFISI YA RAIS

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb.NaEA.7/96/01/K/235                                               8 Julai, 2020

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Bodi ya
Kahawa (TCB), anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi
kuwa usaili wa mahojiano unatarajiwa kufanyika tarehe 16 Julai, 2020.
Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo
yafuatayo:-
i. Usaili wa mahojiano utafanyika tarehe 16 Julai, 2020 kama
ilivyooneshwa kwenye tangazo hili; muda na sehemu ambapo usaili
utafanyika ni kama ilivyoainishwa;
ii. Kila Msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa
amevaa Barakoa (Mask) na kuzingatia masharti mengine ya
kujikinga na COVID 19 KAMA YALIVYOAINISHWA NA WIZARA
YA AFYA awapo eneo la usaili,
iii. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
iv. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na ama Kitambulisho cha
Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi cha taasisi
inayojulikana, Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria au Leseni
ya Udereva;
v. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti
cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, AStashahada, na kuendelea
kutegemeana na sifa za Mwombaji;
vi. Wasailiwa watakaowasilisha “Testimonials”, “Provisional Results”,
“Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha IV na VI
(form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA
HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI;
vii. Kila Msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi;
viii. Kila Msailiwa azingatie tarehe na mahali alipopangiwa kufanyia usaili;
ix. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao
vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (NECTA,
NACTE au TCU);
x. Waombaji kazi ambao majina yao hayaonekani katika tangazo
hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba
tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya
tangazo husika.
xi. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za
Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja
na Leseni za kufanyia kazi.

 

MAJINA // TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI