TANGAZO LA KAZI SERIKALINI – HALMASHAURI YA WILAYA YA IKUNGI

HALMASHAURI YA WILAYA YA IKUNGI

Mkoa wa Singida: S.L.P. 42,
Simu No. 0262964037/6 SINGIDA.
Baruapepe:[email protected]
Tovuti:www.ikungidc.go.tz

Baruapepe:[email protected]

  TANGAZO LA KAZI
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi anapenda kuwatangazia waombaji
wenye sifa nafasi za kazi za Mtendaji wa Kijiji Daraja la III.

 

1. MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III. NAFASI MBILI (02).
Sifa za kuingilia moja kwa moja:
1 Mwajiriwa awe na elimu ya kidato cha nne (IV)au sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya
Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo:
 Utawala, Sheria, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya jamii
kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote
kinachotambuliwa na Serikali.
i. Kazi/Majukumu ya kufanya:
a. Afisa Masuhuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji;
b. Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao, Kuwa Mlinzi wa Amani na
Msimamizi wa Utawala Bora katika ngazi ya Kijiji;
c. Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya
Kijiji;
d. Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji;
e. Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu;
f. Kuandaa Taarifa za Utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha
wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini
na kuongeza uzalishaji mali;
g. Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalam katika Kijiji;

h. Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji;
i. Mwenyekiti wa Kikao cha Wataalamu waliopo katika Kijiji;
j. Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya Wananchi;
k. Kusimamia utungaji wa sheria ndogo za kijiji;
l. Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.

MSHAHARA:
Ngazi ya Mshahara wa Serikali TGS.B.1

 

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KWA WAOMBAJI:-
i. Waombaji wote wawe raia wa Tanzania ambao hawazidi umri zaidi ya miaka 45 na
hawapungui umri wa miaka 18;
ii. Waombaji wote lazima waambatanishe wasifu binafsi (CV) zenye mawasiliano ya
uhakika, anuani, barua pepe na namba za simu;
iii. Waombaji kazi wote wawasilishe maombi yao ya kazi kwa kufuata masharti ya

TANGAZO LA KAZI;
iv.  Waombaji lazima waambatanishe nakala za vyeti vifuatavyo:-
a) Astashahada/Cheti cha Utaalamu kulingana na sifa za nafasi husika.
b) Cheti cha mtihani wa kidao cha nne au sita.
c) Cheti cha kuzaliwa.
v.  Hati ya matokeo ya kidato cha nne (Result slip) haitafanyiwa kazi;
vi.  “Transcript” ambayo haikuambatanishwa na cheti haitafanyiwa kazi;
vii.  Kuwasilisha vyeti vya kughushi na maelezo mengine itasababisha kuchukuliwa hatua za
kisheria;
viii.Watumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba nafasi hizi;
ix.  Waombaji ambao walistaafu kazi kwa sababu yoyote ile hawaruhusiwi kuomba nafasi
hizi;
x.  Waombaji waonyeshe wadhamini wawili na mawasiliano yao, anuani na namba za simu;
xi.  Waombaji wenye vyeti vya kidato cha nne na cheti cha Taaluma ambavyo vimepatikana
nje ya nchi wahakikishe vimehakikiwa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) na Baraza
la Elimu ya ufundi la Taifa (NACTE);
xii.  Barua ya maombi iandikwe kwa Kiswahili au kiingereza.
xiii. Watakaochaguliwa kufanya usaili watajulishwa tarehe ya usaili kupitia tovuti ya
Halmashauri – www.ikungidc.go.tz
4
xiv. Kwa waombaji wenye vyeti vya ngazi ya NTA level 4 “Basic Technician Certificate”
(NTA Level 4) maombi yao hayatafanyiwa kazi. Kwasasa cheti kinachopokelewa ni
“Technician Certificate” (NTA level 5) na kuendelea.

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 23 Juni, 2020 saa tisa na nusu (9:30) Alasiri.
Tangazo hili pia linapatikana kwenye tovuti ya Halmashauri.
Maombi yote ya kazi yatumwe kwa :-

Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi,
S.L.P. 42,
SINGIDA.

(Justice L. Kijazi)
MKURUGENZI MTENDAJI
HALMASHAURI YA WILAYA
IKUNGI

Nakala: Katibu Tawala Mkoa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,
S.L.P 5,
SINGIDA.

Halmashauri zote,
Mkoa wa Singida,
Mbao za matangazo Wilaya na Kata.

 

TANGAZO LA KAZI PDF.