JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb.Na.EA.7/96/01/K/212 6 Juni, 2020
TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Ofisi ya Taifa ya
Ukaguzi (National Audit Office of Tanzania), anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi
wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 13 hadi 17
Juni, 2020 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili
huo.
Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
i. Usaili utafanyika kuanzia tarehe 13 hadi 17 Juni, 2020 kama ilivyooneshwa
kwenye tangazo hili; muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa
kwa kila Kada;
ii. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa
Barakoa (Mask) na kuzingatia masharti mengine ya kujikinga na COVID 19
KAMA YALIVYOAINISHWA NA WIZARA YA AFYA awapo eneo la usaili,
iii. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
iv. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na ama Kitambulisho cha Mkazi,
Kitambulisho cha Mpigakura, Kitambulisho cha kazi cha taasisi inayojulikana,
Kitambulisho cha Uraia ,Hati ya kusafiria au Leseni ya Udereva
v. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha
kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na
kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji;
vi. Wasailiwa watakaowasilisha “Testimonials”, “Provisional Results”,
“Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form V and
form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA
KUENDELEA NA USAILI;
vii. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi;
viii. Kila Msailiwa azingatie tarehe na mahali alipopangiwa kufanyia usaili;
ix. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao
vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (NECTA NACTE na TCU);
x. Waombaji kazi ambao majina yao hayaonekani katika tangazo hili watambue
kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi
zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
xi. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma
wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za
kufanyia kazi.